Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, ametoa siku 14 kwa watu wote walioajiri au kuishi na watu ambao siyo raia wa Tanzania, kujisalimisha kwenye mamlaka husika kabla serikali haijawachukulia hatua kali, akidai kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na wanahatarisha usalama wa nchi.


Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila atangaza vita na wasiooa wala  kuolewa "Ni bakora tu" - Video - Bongo5.com

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.


RC Chalamila, ametoa agizo hilo hii leo Novemba 11, 2020, wakati akizungumza na wafanyakazi wa shirika la ugavi wa umeme nchini, TANESCO tawi la Mbeya, na kusisitiza kuwa wale watakaokaidi kutekeleza agizo hilo, baada ya siku 14 kumalizika watakiona.


“Wale watu wote waliokaa na watu ambao siyo raia wa Tanzania wajisalimishe kwenye mamlaka husika, kuna watu wanaishi na wafanyakazi wa ndani kutoka Malawi, kuna watu ni wahudumu wa hoteli siyo Watanzania”, amesema RC Chalamila.


Katika mkutano wake na wafanyakazi wa TANESCO, RC Chalamila, ametoa maagizo mengine matatu, ikiwemo kuwataka TANESCO kuondoa malalamiko ya wananchi kuhusu kero ya umeme mdogo na wahusika wakaahidi kutekeleza.