LEO Novemba 20 Ligi Kuu Bara inaendelea kwa timu kuingia uwanja kusaka pointi tatu baada ya mapumziko kutokana na majukumu ya timu za Taifa kusaka tiketi ya kufuzu Afcon.

Ratiba ipo namna hii:

Tanzania Prisons  iliyo nafasi ya nane na pointi 15 inawakaribisha Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 12 na pointi 11, saa 8:00 mchana.

Ruvu Shooting iliyo nafasi ya tano na pointi 16 v Mbeya City, iliyo nafasi ya 17 na pointi 7,  saa 10:00 jioni. Uwanja wa Nelson Mandela. Uwanja wa Uhuru.

Dodoma iliyo nafasi ya 11 na pointi 12 v Biashara United,iliyo nafasi ya nne na pointi 17  saa 10:00 jioni. Uwanja wa Jamhuri.