Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameliagiza baraza la mawaziri kufanya kazi kwa weledi ikiwemo kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali za umma kwa maslahi mapana ya Taifa.

Dkt. Mwinyi ametoa maagizo hayo mara baada ya kuwaapisha mawaziri wa awamu ya nane na kuongeza kuwa wahakikishe wanatengezeza mpango kazi utakaoendana na ilani ya chama ikiwemo utakelezaji wa ahadi unaoendana na dira ya maendeleo.

Zaidi, Dkt. Mwinyi amewataka mawaziri hao kuhakikisha wanazijua wizara zao na taasisi zilizoko chini ya wizara husika haraka iwezekanavyo.