Rais Lazarus Chakwera ameagiza kuvunjwa kwa Bodi ya Mitihani baada ya mitihani ya Kitaifa ya mwaka huu kusambaa katika Mitandao ya Kijamii kabla ya Watahiniwa kuifanya.

Mitihani ya Sekondari nchini humo ilipangwa kuanza Oktoba 27 lakini imeahirishwa, hali iliyoleta ghasia za Wanafunzi kuandamana na Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Ikielezwa kuwa Polisi wamewakamata takribani Wanafunzi 38 na Walimu watatu kwa kukutwa na karatasi sita za Mitihani zilizosambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii.

The post Rais wa Malawi Chakwera aamuru bodi ya mitihani ivunjwe baada ya mitihani kusambaa mitandaoni appeared first on Bongo5.com.