Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema kuwa zaidi ya nchi 10 zimetuma salamu za pongezi kwa Rais mteule Dkt Magufuli zikiwemo salamu za Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, China Xi Jinping

”Mpaka sasa tumeshapokea salamu za pongezi kutoka kwa nchi zaidi ya 10 duniani, zikiwemo salamu rasmi za Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, China Xi Jinping ambaye amezitoa kwa rais wetu mteule,” – amesema Dkt Abbas

Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ataapishwa tarehe 5/11 / 2020 Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Dkt Abbas ameongeza kuwa kwa upande wa Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi ataapishwa siku ya Jumatatu ya tarehe 3/11/2020.

 

The post Rais wa China, Xi Jinping ampongeza Dkt Magufuli kwa ushindi (+Video) appeared first on Bongo5.com.