Rais  Magufuli amemuapisha Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania baada ya kuteuliwa Novemba 12, 2020 na kuthibitishwa na wabunge ambao walipiga kura ya ndiyo  kwa asilimia 100.

Pia amewaapisha Dk Philip Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango na Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.

Hafla hiyo ya kuwaapisha wasaidizi wake hao imefanyika leo Novemba 16, 2020, Ikulu Chamwino jijini Dodoma huku ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na wastaafu.