Rais Magufuli amteua Prof. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. John Magufuli amemteua Prof. Adelardius Lubango Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali .
Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imesema uteuzi wa Prof. Kilangi unaanza tarehe 05,Novemba,2020. Prof. Kilangi ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada yakipindi cha kwanza kumalizika jana tarehe tano novemba 2020.