Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amemtumia salamu za heri kwa rais mwenzake wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kushinda uchaguzi uliomalizika hivi punde.
Rais Kenyatta amesema kuchaguliwa tena kwa Magufuli ni ishara ya upendo na imani waliyo nayo Watanzania kwa uongozi wake.
“Kwa niaba ya Watu, Serikali ya Kenya na Mimi mwenyewe nampongeza ndugu yangu, Dkt John Pombe Magufuli kwa ushindi wako na wa Chama Cha Mapinduzi, katika uchaguzi uliomalizika”, alisema rais Kenyatta.
Aliongeza kuandika: ”Nchi ya Kenya inatarajia kuendelea kufanya kazi na Utawala wako kwa faida ya watu wa mataifa yetu mawili, kwa ustawi wa Afrika Mashariki na kwa amani, utulivu na ukuaji wa bara la Afrika.
Rais Kenyatta pia amemtakia rais mwenzake wa Tanzania afya njema na ufanisi anapojiandaa kuhudumu kwa muhula wa pili madarakani na kumhakikishia ushirikiano wa Kenya na kwa utawala wake .
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametetea nafasi yake baada ya kushinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano wiki hii.
The post Rais Kenyatta ampongeza Dkt Magufuli kwa ushindi wa Uchaguzi Mkuu 2020 appeared first on Bongo5.com.