Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Afya katika Wizara ya Afya, Dkt. Jamala Adam Taib kuanzia Novemba 18, 2020.

Aidha, Dkt. Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja, Dkt. Ali Salum Ali.

Dkt. Mwinyi amefikia uamuzi huo baada ya kufanya ziara katika hospitali hiyo ili kujionea mwenyewe hali ya utoaji wa huduma na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.

Kufuatia utenguzi huo, Dkt. Mwinyi amesema wote ambao uteuzi hao umetenguliwa watapangiwa kazi nyingine.