RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi leo tarehe 08 Novemba 2020.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee.
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk.Hussein Ali Mwinyi amemteua ANNA ATHANAS PAUL kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi:-
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 08 Novemba 2020.
Aidha Mheshimiwa ANNA ATHANAS PAUL anatakiwa aripoti Baraza la Wawakilishi leo tarehe 08 Novemba, 2020 saa 6.00 mchana.