SIKU chache baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu kutangazwa, wabunge wengi wameonekana kukosa nafasi kwa mara nyingine kwenda kuwakilisha wananchi kwa kushindwa na wapinzani wao.


Wabunge hao waliokosa nafasi ni pamoja na wanamuziki Joseph Haule ‘Profesa Jay’ aliyekuwa akiwakilisha Jimbo la Mikumi mkoani Morogoro ambapo amepoulizwa kuhusu hatma yake kisiasa na kusema hataki kuongelea mambo hayo ya siasa.


“Kwa sasa siwezi kuongea chochote kile kuhusu siasa, naomba uniache, sijisikii kuongea chochote,” anasema Profesa Jay.