Kampuni kinara ya simu za mkononi ya TECNO, imetoa ofa ya zawadi kwa wateja wake wa kwanza kabisa watakaofanya malipo mapema yaani ku Pre-order simu yake mpya kabisa ya TECNO CAMON 16s ambayo inatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni.
Katika ufafanuzi wake kwenye taarifa ya mpango kazi wa promosheni hiyo ni kwamba mteja atakaye pre-order kwenye maduka yaliyoteuliwa atajinyakulia zawadi za papo kwa hapo zikiwemo TECNO power bank na Wireless Speaker.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba promosheni hiyo inaanza rasmi tarehe 2 Novemba 2020 na itadumu kwa muda wa siku saba yaani wiki moja mpaka tarehe 9 Novemba 2020. Katika kipindi hiki cha wiki moja mteja atatakiwa kutembelea maduka yaliyochaguliwa kufanya promosheni hiyo na kuweka oda ya mapema yaani ku Pre-order.
Simu hiyo ya TECNO CAMON 16s ni simu Bab kubwa ya karne yenye kamera nne nyuma huku kamera yake kuu ikiwa ni ang’avu yenye MP48, Screen kubwa ya inch 6.6 na Storage ya GB 128 ROM + GB4 RAM.
Kufuatia ujio wa simu hii mpya, kampuni ya TECNO imechagua takribani maduka 35 nchini, kufanya promosheni ya Pre-oder katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kagera, Kilimanjaro na Dodoma ili kuwasaidia wateja wake wa mwanzo kupata simu hii bab kubwa kwa bei nafuu pamoja na zawadi, hivyo mteja anaweza kufanya Pre-order katika maduka yaliyoorodheshwa hapo chini pamoja na namba za kuwasiliana moja kwa moja na wahusika. Pia mteja anaweza ku-Pre-order kwa kutumia link hii: https://docs.google.com/forms/d/1zlku0fLU30vvl7L0xWxOkmSRXOPJpl5WzKZSIl1Vwg0/edit
MKOA | DUKA | NO YA SIMU |
DAR ES SALAAM |
Mlimani city, China Plaza, Mobimart, Hyatt, Inobit, RAM 3, RAM 4, Vodacom Mlimani City, Mashreq | 0654843687
0654 304803 |
MWANZA |
Exclusive Jambo Shop, Mbaraka Shop, TECNO Exclusive Katoro Shop, J.B mobile, FAHARI shop | 0719083413
0753144128 |
ARUSHA | Isacky Technology, Happy Shop | 0715092100 |
DODOMA | TECNO Exclusive Pablo shop | 0764161011 |
MOSHI | TECNO Exclusive Totolee | 059392893 |
MBEYA | TECNO Shop Mbeya, BM shop | 0758442496 |
BUKOBA | TECNO Exclusive Bukoba Shop | 0719083413
0753144128 |
The post Pre-order TECNO CAMON 16s Upate Zawadi Papohapo appeared first on Bongo5.com.