Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba amekubali kupokea lawama baada ya kucheza rafu dhidi ya mchezaji wa Arsenal, iliyosababisha penati ambayo iliamua matokeo ya mchezo huo wa ligi kuu ya England.

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba( akiwa chini) baada ya kusababisha penati iliyoipa ushindi Arsenal.

Pogba alinyanyua mguu uliomuangusha Hector Bellerin ndani ya eneo la hatari ambayo aliielezea kama “mjinga”, na Pierre-Emerick Aubameyang akafunga bao lililoipa ushindi The Gunners .

”Tunajua kwamba kilikuwa ni kiwango duni, mimi binafsi sikupaswa kucheza rafu ya aina ile. Nilidhani ningeugusa mpira lakini sikufanya hivyo” alisema Pogba. “Sikupaswa kutoa adhabu mbaya kama hiyo.

Labda nilikuwa nimeishiwa pumzi kidogo, ilinifanya nifanye kosa hili la kijinga. Nitajifunza kutokana na hilo, mimi sio bora kujihami kwenye eneo la hatari, ninaweza kufanya kazi juu ya hilo, “aliongeza kiungo huyo wa Ufaransa.

Manchester United imejikusanyia alama 7 katika mechi 6 ilizoshuka dimbani katika ligi kuu ya England na sasa inashika nafasi ya 15 katika msimamo.

The post Pogba: Nilifanya ujinga mimi sio bora kujihami eneo la hatari, ntajifunza kwa makosa yale appeared first on Bongo5.com.