Klabu ya Plateau United ya nchini Nigeria imegoma ombi la Simba kutaka mchezo wao wa klabu bingwa Afrika kurushwa mubashara.Kwa masikitiko makubwa miamba ya soka nchini Simba imetoa taarifa ya hiyo ambayo itawanyima fursa Wanasimba na Watanzania wote kuushuhudia mtanange huo.

Plateau United wakiwa wenyeji wa mchezo huo watashuka katika uwanja wa New Jos kuwakabili Simba SC majira ya saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Hapo jana tumeshuhudia wawakilishi wingine wa kimataifa klabu ya Namungo wakipeperusha vema bendera ya Tanzania katika michuano ya Shirikisho baada ya kuwafunga Al Rabita jumla ya magoli 3 – 0 mchezo uliyopigwa hapa nchini huku mchezaji Steve Sey akitupia mawili na Shiza Kichuya akihitimisha karamu ya magoli.