Katika kuhitimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja, Benki ya NMB, imewakutanisha na kuwapa watoto zaidi ya 25
elimu kuhusu masuala ya kuweka akiba na nidhamu ya fedha. 

Akizungumza wakati wa utoaji elimu huo, ulioambatana na ufunguaji wa akaunti mbalimbali zilizo chini ya mwamvuli wa WAJIBU, Meneja wa NMB Tawi la Oyster Plaza – Hildegard Mung'ong'o, alisema elimu waliyopewa watoto hao ililenga kuwajengea utamaduni endelevu wa kuweka akiba tangu wakiwa wadogo.

Meneja wa NMB Tawi la Oyster Plaza – Hildegard Mung'ong'o akiangalia jinsi mtoto Myreen Rashid akiweka pesa ikiwa ni sehemu ya kujifunza kuhusu kuweka tangu wakiwa watoto.

Hildergard alibainisha kuwa, Tawi lake pamoja na matawi yote ya NMB nchini huwa yanajisikia Furaha kukutana na
watoto pamoja na wazazi kuwapa elimu juu ya masuala ya kifedha (WAJIBU) inayojumuisha akaunti tatu za Mtoto
Akaunti, Chipukizi Akaunti na Mwanachuo Akaunti.

 

The post NMB yafunga mwezi wa huduma kwa wateja kwa kuwanoa watoto appeared first on Bongo5.com.