Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya  Chama cha Mapinduzi  CCM ambayo iliketi jana Dodoma  imempongeza Rais John Magufuli kwa kushinda kiti cha urais kwa muhula wa pili ya mwaka 2020-25.

 

Pia imewapendekeza Job Ndugai kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Tulia Ackson kuwania Naibu Spika na Zuber Alli Maulid kuwania Spika wa Baraza la Wawakilishi.