Ndege kubwa zaidi zilizowahi kutengenezwa duniani (+Picha)
Tangu binadamu alipofanikiwa kuunda ndege na kupaa angani, wataalamu wamekuwa wakijitahidi kuunda ndege kubwa na kubwa zaidi.
Wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia, majaribio ya kwanza ya kuunda ndege kubwa zaidi yalifanyika.
Ndege hizo zilikuwa na injini kadha, na zilikuwa na uwezo wa kubeba na kuangusha mabomu mengi.
Kabla ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kuliundwa ndege kama vile Dornier Do X ambayo ilikuwa kama meli kubwa na ndege ya ANT-20 ya Muungano wa Usovieti ambayo ilikuwa kubwa ajabu.
ANT-20 ilikuwa na uzani wa tani 50 ilipokuwa inapaa, na mabawa yake yalikuwa na urefu wa futi 207 (mita 63). Ndege hii ilikuwa na chumba chake cha kupigia chapa, ukumbi wa sinema na chumba cha kutolea picha.
Kuundwa kwa injini ya jeti kuliwezesha ndege kubwa na nzito zaidi kuundwa.
Ni hapo ambapo ndege kubwa kama vile Airbus A380, ndege ya ghorofa yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 850 ziliundwa.
Kuliundwa pia Antonov An-225, ndege kubwa ya mizigo ambayo inaweza kubeba mizigo ya tani 250. Ndege hiyo ni kubwa kuliko ambali ambao ndege ya kwanza ya Ndugu ya Wright ilisafiri mara ya kwanza ilipofanikiwa kupaa.
Hapa chini ni mkusanyiko wa baadhi ya ndege kubwa zaidi kuwahi kuundwa.