Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametangaza kupata tiba ya Corona Virus ambayo imegunduliwa na Wanasayansi wa Uganda

Katika hotuba yake kwa Taifa jana Jumapili, Museveni amesema Madaktari wanatumia mchanganyiko wa vitu maalum ambavyo vinaongeza kinga mwilini

Dawa hiyo ambayo amesema itaanza kutumika Desemba 15, imejaribiwa kwa Wagonjwa kadhaa wa COVID 19 nchini humo na wamepona

Pia, Wanasayansi wamegundua namna ya kupima COVID19 kwa kutumia mate ambapo majibu hutoka ndani ya dakika 30