Mnyama Simba aunguruma Nigeria, akamilisha kazi aliyotumwa
Wawakilishi hao wa nchi kimataifa #simbasc imefanikiwa kuondoka na ushindi huo wa goli 1 – 0 dhidi ya wenyeji wao timu ya Plateau United mchezo uliyopigwa katika dimba la New Jos nchini Nigeria.
Kwa matokeo hayo sasa Bingwa huyo mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara anarejea nyumbani kujipanga kwaajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa katika uwanja wa Mkapa kati ya tarehe 4-9 mwezi Disemba 2020