Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameanza kujitenga baada ya kukutana na mtu aliyebainika kupata maambukizi ya virusi vya corona.

Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema yeye binafsi hakuwa na dalili za corona.

“Mtu niliyekutana naye hivi karibuni amebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona. Niko sawa na sina dalili zozote lakini nitajitenga kwa siku kadhaa zijazo, kama ilivyo katika muongozo wa WHO, na kufanya kazi nyumbani,” ameandika kwenye ujumbe wa Twitter.

“Wafanyakazi wenzangu wa WHO na mimi tutaendelea kushirikiana na wengine kuokoa maisha na kulinda maisha ya walio hatarini,” aliongeza.

Dkt.Tedros mwenye miaka 55, alikuwa waziri wa afya nchini Ethiopian alisema “ni muhimu sana kufuata muongozo wa wizara ya afya”. “Kwa njia hii, ndio tutafanikiwa kukabiliana na usambaaji wa ugonjwa wa Covid-19 kukabiliana na kirusi hichi, na kulinda mifumo ya afya.”

Dkt Tedros, kama anavyopenda kufahamika, ni kiongozi wa kwanza wa Afrika katika shirika la WHO.

The post Mkuu wa WHO Tedros Adhanom yuko karantini kisa Corona appeared first on Bongo5.com.