Na Faruku Ngonyani , Mtwara

Wavuvi Mkaoni Mtwara wameelezea changamoto zao ikiwepo pomoja na ukosefu wa mikopo kutoka katika Taasisi za kibenk hapa nchini hali inayopelekea kutokuwa na vifaa bora vya Uvuvi.

Hayo yamezungmzwa na Abasi Salum Waziri ambaye ni katibu wa BMU n msemaji wa wavuvi katika soko la Feri na ameyazungumza hayo wakati wa ufunguzi wa kuelekea  siku ya wavuvi hapa nchini tarehe 21 Novemba 2020 mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstani Kyobya.

Abasi Salum amesema kuwa licha ya mikopo amezataja changamoto zingine ikiwa ni pamoja na sheria za uvuvi zimekuwa ukilinganishwa na uelewa wa wavuvi hao

“Mhe Mkuu wa Wilaya juzi tu hapa Mh Raisi amezindua bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania tunagemea wabunge watatengeneza sheria ambazo zitakuwa rafiki kwa wavuvi sisi,mkuu wa Wilaya yachukue haya tunajua raisi wetu msikivu sana”

Kwa upande wake Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstani Kyobya amezitaka Taasisi za fedha na Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani pamoja Wilaya ya Mtwara kuwatembelea wavuviu na ktoa elimu ya kutosha juu mikopo pamoja na  kuwaeleza utaratibu wa upatikanaji wa Mikopo yenyewe.

Ikumbukwe siku ya wavuvi Duniani huadhimishwa kila inapofika tarehe 21 Novemba kwa kila mwaka na kwa mkoa wa Mtwara maadhimisha hayo yatafanyika katika viwanja vya soko la feri vilivyopo Manispaa Mtwara Mikindani.