Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ni kati ya viongozi wa upinzani walioachiwa kwa dhamana leo Jumanne Novemba 3, 2020.


Wengine walioachiwa ni wajumbe wa kamati kuu ya Chadema,   Godbless Lema na Boniface Jacob ambao pamoja na Mbowe walikamatwa na polisi usiku wa kuamkia Novemba 2, 2020 wakiwa kwenye kikao. Zitto alikamatwa leo mchana alipokwenda kuwatembelea kina Mbowe polisi.


Wakili wa Chadema John Mallya amesema viongozi hao wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti polisi Novemba 5, 2020 saa 3 asubuhi.


Mallya amesema viongozi hao wameachiwa baada ya kujidhamini wenyewe na kutakiwa kutotoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam na kuhakikisha wanaripoti kituoni hapo tarehe waliyopangiwa