“Hatutamruhusu yeyote kutuzuia kutekeleza jukumu letu la kuhesabu kura,” hayo ni maneno ya Joe Gloria, msajili wa eneo la Clark huko Nevada, amewaambia wanahabari.

Amesema maafisa wa usalama wamepelekwa eneo hilo huku hatua zingine za kiusalama zikichukuliwa kuhakikisha wafanyakazi wako salama kuendelea na shughuli ya uhesabuji wa kura.

Lakini pia ameongeza kuwa masanduku ya mwisho ya kura yanayotarajiwa kuwasilishwa baadae huenda matokeo yakatolewa wiki ijayo kabla ya matokeo kamili kufahamika.

Joe Biden sasa hivi anaongoza kwa kura kidogo huko Nevada, na kampeni ya Trump imetishia kuwasilisha kesi ya madai ya udanganyifu mahakamani ingawa hadi kufikia sasa hakuna ushahidi wowote uliotolewa.

Akijibu madai ya udanganyifu wa kura, Bwana Gloria alisema: “Hatufahamu lolote kuhusu uhesabu wa kura zisizostahili.”

The post Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020: Usalama waimarishwa katika kituo cha kuhesabu kura Nevada hali sio shwari appeared first on Bongo5.com.