Hizi ni 'updates' kuhusu tukio la kupata ajali kwa msanii wa BongoFleva Kusah ambalo imempelekea kuvunjika mguu wake wa kulia, ambapo siku ya leo ameshea video fupi ikionyesha gari ambalo amepata nalo ajali kupitia mtandao wa Instagram.


Kupitia video hiyo Kusah ameandika kuwa "Huyu Mungu wetu ni mwema sana, kuna muda nakaa nalia  maana maumivu hayazoeleki ila kila nikifikiria ajali iliyotokea na mimi nilivyo bado najiona mwenye bahati kubwa, Ahsante Mungu kwa hili naamini ipo siku nitasimama tena inshaallah"