Mbunifu wa mitindo @martinkadindaofficial amefunguka kumzungumzia rafiki yake wa karibu Mwanamitindo na video queen, Jack Cliff ambaye amefungwa nchini China mwaka 2013 kutokana Dawa za Kulevya.

Mbunifu huyo ambaye alionekana sana kuumizwa na hali ya mrembo huyo alisema mara ya mwisho wakati anazungumza naye alikuwa anauliza mambo mengi ya kimaendeleo.

Martin ambaye hivi karibuni alimpost mrembo huyo, amesema mara ya mwisho Jack alitamani kununua vitu vya urembo ili akirudi avitumie lakini akakuta vimeisha.

The post Martin Kadinda afunguka alichozungumza na Jack Cliff aliyefungwa China (Video) appeared first on Bongo5.com.