Taifa la Marekani linaendelea na mchakato wake wa kuhesabu kura za kuwachagua wawakilishi wa miji, majimbo na Urais kutokana na uchaguzi uliofanyika tarehe 3 Novemba, macho ya Wamarekani na wasio kuwa wananchi wa taifa lao, wanatizama kwa karibu kinyang'anyiro cha matokeo ya Urais,

 

 mathalani kwa wagombea wawili Donald Trump (Republic) na Joe Bidden (Democrat) ambao wanachuana kwa ukaribu sana.


Katiba ya Marekani inamruhusu Rais kukaa vipindi viwili madarakani ambapo kila muhula una miaka minne hivyo kuwa miaka minane, japo imekuwa ni nadra sana kwa miaka ya hivi karibuni Rais wa taifa hilo kushindwa muhula wa pili na hiyo haimanishi kuwa haiwezekani kwani historia inaonesha kuwa wapo Marais ambao waliongoza muhula mmoja kutokana na kushindwa katika chaguzi za kuwania muhula wa pili.


Jumla ya Marais 11 wa Taifa hilo wameshindwa katika chaguzi mbalimbali za kuusaka muhula wa pili wa kuingia Ikulu ya Marekani (White House). Miongoni mwa Marais hao ni George H.W. Bush Sr (Republic) Rais wa 41 ambaye alihudumu kutoka 1989-1993 baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 1992 dhidi ya William Jefferson Clinton (Democrat).


Jimmy Carter (Democrat) Rais wa 39 (1977-1981), Gerald R. Ford (Republic) Rais wa 38 (1974 - 1977), Herbert Hoover (Republic) Rais wa 31 (1929-1933), William Howard Taft (Republic) Rais wa 27 (1909-1913), Benjamin Harrison (Republic) Rais wa 23 (1889-1893),Grover Cleveland (Democrat )Rais wa 22 na 24 (1885-1889), Martin Van Buren (Democrat) Rais wa 8 (1837 -1841), John Quincy Adams,Rais wa 6 (1825-1829), John Adams (Federal), Rais 2 (1797-1801). hii ni kwa mujibu wa ThoughtCo.


Swali linabaki kuwa je Trump atakiruka kihunzi cha kuishia muhula mmoja ?, majibu ya swali hilo yanausubiri tu mshale wa saa ambao ndiyo utaamua kama ni Trump au Bidden. Na matokeo haya yataamua Trump kuendelea  kuwa Rais wa 45 ama Bidden kuwa Rais wa 46.