Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetabiri uwezekano wa kunyesha mvua kubwa katika mikoa minane ya Tanzania ambazo zinaweza kusababisha mafuriko mkatika baadhi ya maeneo.

Mikoa hiyo ni Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe.

Akizungumza leo Jumapili Novemba 15, 2020, mchambuzi wa TMA, Joyce Makwata amesema mvua hizo zinatarajiwa kunyesha ndani ya saa 24 katika mikoa hiyo ambapo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhali.

Makwata amesema mvua hizo zitasababisha baadhi ya makazi ya watu kuzungukwa na maji na barabara kutopitika.

Amesema wananchi wa maeneo hayo wanatakiwa kuchukua hatua hasa wale wanaoishi mabondeni na wafuatilie mara kwa mara taarifa za TMA.