Joe Biden, ambaye alikuwa makamu wa rais chini ya Barak Obama, aliweza kupata uungwaji mkono wa majimbo muhimu ambayo mwaka 2016 yalimpigia kura hasimu wake wa Republican Donald Trump.
Akikaribia kutimiza umri wa miaka 78, Biden atakuwa ndiye rais mwenye umri mkubwa zaidi wa Marekani.
Tunakueleza mambo mengine ya kipekee kuhusu maisha ya kibinafsi na ya kitaaluma ya Biden.
1. Ni mwanasiasa aliyesomea
Kama Trump alijvyosisitiza katika kumkumbusha wakati wote wa kampeni, Bwana Biden amekuwa mshiriki wakati wote katika siasa za Marekani kwa miaka 47.

Kazi yake ya siasa katika Washington DC ilianza katika Seneti ambapo alishinda kiti cha jimbo la Delaware alipokuwa na umri wa miaka ya thelathini na zaidi, alikabiliwa na moja ya nyakati za kusikitisha zaidi za maisha yake na hili tutalizungumzia baadaye katika taarifa hii.
Kama Seneta, Biden aliimarisha sura yake kama mwanasiasa wa karibu, mpatanishi na mwenye uwezo wa kufikia makubaliano na wapinzani wake.

Pia alifanya maamuzi ambayo hayakusifiwa sana na wengi, kama vile sheria ya uhalifu aliyoandika na kupitishwa wakati wa utawala wa kwanza wa Bill Clinton.
Sheria hiyo ilikuwa ya mageuzi yaliyolenga kukabiliana na ghasia za miongo kadhaa , lakini ilisababisha kunyanyaswa kwa watu wengi , huku ikiwaathiri zaidi Wamarekani weusi na Walatino.
Katika kipindi kirefu cha kazi yake kama seneta, hatunabudi kuongeza miaka yake minane ya kuwa Makamu wa rais wa Barack Obama (2009-2017), ambapo alijenga uhusiano mzuri naye zaidi ya uhusiano wa kikazi.

Hii ni mara ya tatu akijaribu kupata urais wa nchi.
Mara mbili za kwanza aligonga mwamba, akisababisha baadhi ya Wanademocrat kujiuliza iwapo kweli alikuwa mtu anayefaa kukabiliana na Trump.
2. Tukio la kusikitisha lilimpata katika mwanzo wa kazi yake ya kisiasa
Kwa bahati mbaya, furaha ya kushinda uchaguzi wa Seneti haikudumu kwa muda.
Wiki kadhaa baada ya ushindi wake, familia yake ilihusika katika ajali mbaya ya gari wakati alipokuwa Washington, DC, akiwafanyisha mtihani watahiniwa ambao wangekuwa wahudumu wa ofisi yake.
Mke wake Neilia na watoto wao watatu walikuwa wakirejea nyumbani baada ya kutoka dukani kununua mti wa Krismasi wakati lori lilipowagonga na gari lao.
Mke wake aliyekuwa na umri wa miaka 30 na binti yao, Naomi aliyekuwa na miezi 13, walifariki.

Watoto – Beau, aliyekuwa na miaka 3, Hunter, miaka 2, walijeruhiwa sana na kulazwa hospitalini .
3. Maumivu na huruma
Biden, ambaye alikula kiapo cha kuwa Seneta katika chumba cha hospitali ambako mwanae wa kiume Beau alikuwa anatibiwa, hakuweza kujua kama angeweza kuendelea na kazi yake kama seneta
Nilikuwa nimefikia mwisho sikujua la kufanya
Akizaliwa katika familia ya wafanyakazi wenye imani ya Kikatoliki, baba yake alirejelea maneno haya lakini akimlazimisha : “Amka, amka baada ya kuanguka . “
Hicho ndicho alichokifanya. Aliamua kujitupa katika kazi, lakini bila kuwaacha watoto wake.

Moja ya mambo yaliyojitokeza zaidi katika miaka yake ya mwanzo kama seneta ni kwamba : kila siku alilazimika kusafiri kati ya nyumbani Delaware Washington DC, zaidi ya kilomita 300 kwa siku ili kuwa karibu na watoto wake.
Biden aliendeleza uhusiano wa karibu na watoto wake ambao uliimarika walipokuwa watu wazima.
Mwaka 1977, Biden alimuoa Jill, profesa wa Chuo Kikuu ambaye alizaa naye mtoto wa kike , Ashley, na kuweza kushirikiana naye kuijenga familia.
Wengi walimuona Beau kama mtu anayeweza kumrithi baba yake katika siasa.
Baada ya kuhudumu nchini Iraq na kikosi cha walinzi wa taifa -National Guard mwaka 2008, Beau alikuwa Mwanasheria Mkuu wa jimbo la Delaware kwa mihula miwili akiwa na matumaini mazuri ya kikazi kwa siku zijazo .

Lakini mwaka 2013 alipatikana na saratani nadra ya uvimbe wa kwenye ubongo na akafariki miaka miwili baadaye.
Kumpoteza mtu wake wa karibu kiasi hicho kulibadili tabia ya Biden.
Wale wanaomfahamu zaidi wanasema kuwa mtu mwenye “uwezo mkubwa wa kuhurumia “, jambo lililotumiwa zaidi wakati wa kampeni yake akielezewa kama mtu anayeweza kuwa rais anayeweza kukabiliana na mizozo ya kiafya, kiuchumi na kijamii kama vile janga la Covid -19.
4. Raia wa dunia na aliyejitolea kuilinda sayari
Biden ametetea haja ya kujenga upya uhusiano wa Marekani na nchi washirika wake ambazo, kwa maoni yake, umeathiriwa wakati wa urais wa Trump.
Aliahidi kurejea katika mapatano ya Paris ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na Shirika la afya duniani.

Maamuzi yake katika ngazi ya kimataifa yamekuwa yakikosolewa.
Mwaka 1991 alipiga kura dhidi ya Vita vya Ghuba; hatahivyo, katika mwaka 2003 aliunga mkono uvamizi wa Iraq na baadaye akawa mkosoaji wa harakati za Marekani katika nchi hiyo.
Akiwa mtu mwenye umakini, alimshauri Obama kutofanya opereshini maalumu iliyosababisha kifo cha Osama Bin Laden.
5. Mtu anayeweza kusababisha utata
Wakosoaji wa Biden wanasema ni miongoni mwa watu ambao wamepitwa na wakati na mzee sana ambaye hawezi kuongoza ofisi ya rais akiwa na tabia ya kufanya makosa.
Mtindo wake wa kuwa mkweli na kuchukulia mambo kwa urahisi umemsababishia matatatizo kama vile aliposema kuwa katikati ya kampeni kwamba kama Mmarekani mweusi hajaamini kuwa anaweza kumpigia kura ina maanisha kuwa huyo sio mweusi, kauli ambayo baadaye ilimlazimu aombe radhi kwa kuitoa.

Tabia yake ya “usumbufu” ilibadilika na kuwa kitu kikubwa baada ya mwezi Machi msaidizi wake wa zamani , Tara Reade, kudai kuwa rais mteule alimnyanyasa kingono miaka 30 iliyopita wakiwa Washington.
Biden na timu yake walipinga shutuma hizo na kesi hiyo iliishia patupu bila kuwa na umuhimu wowote wakati wa kampeni

Ingawa mahasimu wake wa Republican walijaribu kumuonesha mwanaume mwenye matatizo makubwa ya ubongo ambaye yuko mikononi mwa wanachama wa mrengo wa itikadi kali za kushoto wa Democrat, Biden ameweza kuepuka hayo na kuwa rais aliyechaguliwa zaidi katika historia ya Marekani.
La kushangaza, wakati ilipofanywa tathmini miaka kadhaa iliyopita juu ya iwapo anaweza kushauriwa kushiriki katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 , Biden alisema: “Ninaweza kufa nikiwa mwanaume mwenye furaha bila kuwa rais . “
The post Mambo 5 ambayo huenda huyafahamu kuhusu rais mteule wa Marekani Joe Biden appeared first on Bongo5.com.