MAMA mzazi wa staa mkubwa wa muziki barani Afrika na bosi wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’, amewajibu wanaomtaka amzalie mtoto mumewe, Maisara Shamte ‘Uncle Shamte’.

Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram, Mama Dangote alimjibu shabiki mmoja aliyemuuliza mbona habebi mimba? Mama huyo mwenye zaidi ya umri wa miaka 50 alimjibu; “Siko kwenye kubeba mimba, mimi ni bata kwa kwenda mbele!’’

Hata hivyo, katika majibizano hayo, wapo waliompongeza kwa kujibu hivyo kwani watu wengine wanakera na maswali yao. “Huyo ndiye Mama Simba (Mondi) bwana, vizuri sana, wakomeshe wenye midomo yao…’’ aliandika shabiki mmoja kwenye ukurasa wa Mama Dangote. Shabiki mwingine alijibu kuwa, umri wa Mama Dangote umeenda hivyo hawezi kushika tena mimba.

Baada ya mambo kuwa mengi mtandaoni, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilimtafuta Mama Dangote ambapo alisema kuwa hataki umbeya na kukata simu.

“Mimi sitaki mambo ya udaku kabisa hata kama nimejibu hivyo,’’ alijibu na kukata simu. Mama Dangote amekuwa akishambuliwa na baadhi ya mashabiki hasa anapoposti picha akiwa na mumewe huyo. Hata hivyo, wapo ambao wamekuwa wakimpongeza kutokana na jinsi yeye na mumewe wanavyopendana kiasi cha kuwanyima usingizi wananzengo.


STORI: HAPPYNESS MASUNGA, DAR