Mtangazaji mahiri nchini, mwenye sauti ya aina yake, #Diva ameweka wazi sababu ya yeye kutofautiana na msanii #DiamondPlatnumz hadi kufikia hatua ya kupelekana Mahakamani.


Kwenye mahojiano na Zamaradi, #Diva amesema hilo lilijiri baada ya kusikia msanii huyo kusema aliomba kazi kwenye Kituo chake cha Radio na kumkatalia.


#Diva aliendelea kueleza kwamba sababu nyingine ni yeye kuwa upande wa Msanii Alikiba (kwakumsapoti) na #Diamond hakupenda. Diva ameiambia Zamaradi Tv.


Licha ya hayo, #Diva pia alisisitiza kusema anampenda Msanii #Alikiba na ni shabiki mkubwa wa nyimbo zake.