Madereva watatu wa kike wa magari makubwa ambao wameunda kikundi chao wameungana kwa ajili ya kulaani maandamano yaliyopangwa kutokea nchini.

Maandamano hayo ambayo yalipangwa na viongozi wa juu wa vyama viwili vya Siasa CHADEMA na ACT WAZALENDO kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo tarehe 28/10/2020 nchini Tanzania.

Madereva hao wamesema kuwa endapo yakitokea maandamano waathirika wakubwa ni wanawake na watoto hivyo wakiwa kama madereva wanawake na mama wenye familia wanajitokeza wakiwakilisha wanawake wengine kulaani maandamano ambayo yatakuja kuathiri amani ya Tanzania.

Wameongeza kuwa Vijana wasikubali kutumiwa na wanasiasa kwa ajili ya manufaa yao binafsi.

 

The post Madereva wa kike wa magari makubwa, walaani maandamano Tanzania, waathirika wakubwa wanawake na watoto (+Video) appeared first on Bongo5.com.