MREMBO anayefanya vizuri kwa sasa kunako gemu la Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ amesema kuwa wambea wanaofuatilia mapenzi yake na mpenzi wake wa sasa Awadhi Masomo wanapoteza muda wao bure ni bora wampotezee.

 

Akipiga stori mbili tatu na Mikito Nusunusu, Linah alisema kwamba, kwa mwanaume huyo ndio amefika kwani ana kila kitu alichokuwa anakihitaji hivyo hatarajii kuachana naye kabisa.

 

“Mwenzenu hapa ndio nimefika, mpenzi wangu ananipa raha zote za dunia, najinenepea tu, kuna watu wanatuhesabia siku mimi naona wanapoteza tu muda wao, kwa sababu hatutarajii kuachana leo wala kesho, Awadhi ndio mume wangu, nitamzalia na mtoto yaani kwa ufupi hatuachani ng’oo,” alisema Linah.

 

Kabla ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume huyo, Linah amewahi kubanjuka kimapenzi na msanii mwenzake Amini Mwinyimkuu kabla ya kuhamia kwa Shaban Mchomvu aliyezaa naye mtoto mmoja wa kike aitwaye Tracy.


STORI: MEMORISE RICHARD