Rais mteule wa Marekani Joe Biden amelaani kitendo cha Donald Trump kukubali kuwa ameshindwa katika uchaguzi wa rais, amesema kuwa 'anatuma ujumbe mbaya sana kuhusu Marekani'.

Bwana Biden amesema, alikuwa na uhakika kuwa bwana Trump alikuwa anajua kuwa hasingeshinda na kila kitu kilionekana wazi , kwa kuwa alikuwa hajitumi kabisa katika majukumu yake.

Kulikuwa na marudio ya kuhesabu kura za uchaguzi wa rais katika jimbo la Georgia, na bwana Biden alipata ushindi katika jimbo hilo.

Bwana Trump alifungua kesi ya madai ya wizi wa kura.

Madai yake yote ya kisheria yaligonga mwamba na kushindwa kufanya mabadiliko yoyote.

Bwana Biden amepata ushindi wa kura za umma kwa zaidi ya milioni 5.9 .

Ushindi wake katika kura za wajumbe ambazo zinaweza kuthibitisha nani anakuwa rais aliweza kukadiriwa kupata kura 306 mpaka 232

Alikuwa akiongea katika mkutano wa simu na magavana , wakiwemo wa Democrats na Republicans, kuhusu janga la corona.

Alihojiwa kuhusu suala la Trump kutokubali ushindi wake, Biden alisema rais anatuma ujumbe wa kutisha... kwa dunia nzima kuhusu jinsi demokrasia inavyofanya kazi, na hilo anapaswa kulikumbuka kwa kuwa amekuwa rais ambaye hawajibiki katika historia ya Marekani."