VYUMA vimekaza! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mwanamama na staa wa fi lamu za Kibongo, Irene Uwoya, kufunga baa yake ya Last Minute iliyopo Sinza, Dar, huku sababu zikiwa hazijulikani.

Baa hiyo ambayo mbali na kazi yake ya fi lamu, ndiyo ilikuwa ikimuingizia kipato na kumpa jeuri mjini hapa mwanamama huyo, ilifungwa huku taarifa nyingi zilikuwa zikisambaa zikianisha sababu za kufungwa kwa baa hiyo.

VYANZO VINASEMAJE


Taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali zimesema kuwa, msanii huyo alikosa mtaji wa kuendesha biashara yake na ndiyo sababu akaamua kuifunga. “Hana lolote zaidi ya kufulia na kukosa mtaji wa biashara japo anafi cha tu,’’ kilisema chanzo kimoja kilichoomba kuhifadhiwa jina lake.

Haikuishia hapo mmoja wa watu wake wa karibu na Uwoya ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini, aliliambia Gazeti la Amani kuwa, Uwoya kakosa kodi ya kulipia pango na hata kwenye mapato ya serikali na ndiyo maana akaamua kuifunga.

“Sababu kubwa ya Uwoya kuifunga hiyo baa ni kutokana na kukosa kodi ya kulipia hasa kwenye mapato ya serikali (TRA), maana si unajua tena huwa kuna kodi ya pango na biashara, hicho ndicho kilimshinda na ustaa wake,’’ alisema mtu wa karibu na Uwoya japo naye hakutaka jina lake lichorwe magazetini.

UWOYA AFUNGUKA

Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Uwoya ili aweze kuzungumzia ishu hii ambapo alisema kuwa, hivi karibuni ataifungua tena baa yake.


“Mimi naona biashara zangu ziko poa, Last Minute ipo na tutaifungua hivi karibuni japo Corona ilisababisha tuifunge.


“Kuhusu watu kusema nimeifunga au nimefulia, si kweli maana maneno yanazungumzwa na huwezi kuwazuia watu kuongea lile wanalotaka kuongea, mi niseme watu wasubiri waone,’’ alisema Uwoya huku akisistiza kuwa hajafulia.

KUHUSU VYANZO VYAKE VYA PESA


Baada ya kuzungumzwa kuhusiana na wapi anatoa pesa za kutanua na kula bata ilihali baa yake imefungwa ambapo alisema kuwa, ana bishara zingine.


“Maisha yangu ni ya kawaida si wkamba kuna sponsor na sijawahi kubadilika, pia nina biashara zingine ninazozifanya na zinaniingizia pesa,’’ alimalizia kwa kusema.


Mbali na kuifunga biashara hiyo, Uwoya amekuwa akisifi ka kula bata na kumiliki kiwango kikubwa cha pesa huku vyanzo vyake vikiwa havijulikani. Hivi karibuni Uwoya alizindua reality show yake inayokwenda kwa jina la I AM EVERY WOMAN ambayo inazungumzia maisha ya yake halisi.