Bodi ya ligi Tanzania (TPBL) imefanya mabadiliko ya ghafla kwenye ratiba ya mchezo mmoja, ambapo mabadiliko hayo yameonesha kuziumiza baadhi ya timu.

 

Kwa mfano timu ya Ruvu Shooting iliyopaswa kucheza na Mwadui ya Shinyanga tarehe 07/11/2020, kwenye ratiba ya awali ghafla wakapewa taarifa mechi yao kuchezwa Jumatano tarehe 4/11/2020 .hivyo wakalazimika kuanza safari saa 5:00 asubuhi siku ya Jumanne kwa njia ya barabara


Bodi ya ligi inayoongozwa na Mwenyekiti wake Steven Mguto, imekuwa kwenye lawama za mara kwa mara juu ya mabadiliko ya ratiba katika ligi madaraja yote wanayo simamia


Uteuzi wa Almas Kasongo kushika nafasi ya mtendaji mkuu wa bodi hiyo, kulileta imani kubwa ya kutatua tatizo la ''pangapangua'' za mara kwa mara kutokana ma uzoefu na uweledi wake katika mchezo wa soka


Ikimbukwe kuwa hata mchezo mkubwa wa ligi ya Tanzania, inayohusisha Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi tarehe 7 uwanja wa kumbukumbu ya Hayati Benjamin Mkapa, awali ulipaswa kuchezwa Oktoba 18, lakini ukaahirisha na sasa unategemewa kuchezwa Jumamosi hii