Mwaka 2013 Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Nigeria iliwahi kutoa adhabu kwa klabu nne kwa tuhuma za upangaji matokeo.

Zikihitaji kuhakikisha zinapanda daraja timu mbili za Plateau United na Police Machine zilihakikisha zinakuwa na mabao mengi ili kuwa na tofauti ya magoli na kuzidiana.

Ndipo Plateau United ikifunga magoli 72 – 0 katika kipindi cha kwanza kisha kufikisha jumla ya mabao 79-0 dhidi ya Akurba FC ndani ya dakika 90.

Wakati huo huo mpinzani wake ambaye ni klabu ya Police Machine ikachomoza na ushindi wa jumla ya magoli 67-0 dhidi ya Babayaro FC ambapo kati ya hayo goli 7 zikifungwa dakika 45 za kipindi cha pili.

Kufuatia tukio hilo ndipo Shirikisho la soka Nigeria ikasema matokeo hayo ni haibu na kufanya uchunguzi uliyopelekea baadhi ya viongo, wachezaji kufungiwa maisha huku baadhi ya klabu kupewa adhabu kali.

The post Kisa cha FC Plateau United mpinzani wa Simba kushinda goli 79 – 0 dhidi ya Akurba FC (+Video) appeared first on Bongo5.com.