Rapa Lil Wayne afunguliwa mashtaka ya kumiliki silaha yenye risasi, ambalo ni kosa la jinai. Kama akikutwa na hatia ya kosa hilo, Weezy huwenda akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.


Shtaka hilo limefunguliwa kwenye Mahakama ya wilaya mjini Florida likimtaja Dwayne Michael Carter Jr, maarufu Lil Wayne akituhumiwa kukutwa na silaha yenye risasi kwenye begi akiwa kwenye ndege yake binafsi, Disemba mwaka jana.


Disemba 11 mwaka huu ndio itakuwa siku ya kwanza kwa Lil Wayne kuhudhuria mahakamani, ikumbukwe pia Wayne ana tuhuma za kumiliki silaha kinyume cha sheria mwaka 2009 mjini New York.