MGOMBA urais nchini Uganda, Patrick Amuriat, amekamatwa katika mji mkuu wa Kampala katika makao makuu ya chama chake cha Forum for Democratic Change (FDC).

 

Wanajeshi na maafisa wa polisi walikuwa wamezungumza ofisi za chama chake kwa mujibu na  gazeti la Daily Monitor.

 

Amuriat alikuwa amekiuka masharti yaliyowekwa na tume ya uchaguzi nchini humo ya kufika kwenye shughuli ya uteuzi na wagombea 10 pekee ambao amepangiwa kuwasilisha makaratasi yake kwa ajili ya uteuzi leo mchana.

 

Msimamo wa chama hicho ulitolewa licha ya jeshi la polisi jana usiku kusema kuwa liko tayari kukabiliana na yeyote atakayekiuka masharti ya tume ya uchaguzi.