Kimbunga Eta kimeipiga pwani ya Nicaragua na kusababisha uharibifu pamoja na vifo vya watu wawili ikiwemo mtu mmoja katika taifa jirani la Honduras.

Hurricane Eta slams Nicaragua as Category 4, 'extremely dangerous' storm | Fox News

Kitovu cha kimbunga Eta kiliwasili kiasi kilometa 26 kusini ya wilaya mashuhuri ya Puerto Cabezas kikiwa na kasi ya kilometa 220 huku kikiambatana na mvua kubwa iliyosabasiaha maporomoko ya udongo kwenye mgodi yaliyomuua mtu mmoja.

Kimbunga hicho, ambacho watalamu wamekiorodhesha kuwa hatari, kimeangusha miti, kuharibu miundombinu ya kusambaza umeme, kuezua mapaa ya nyumba na kusababisha kufurika kwa mito kaskazini ya Nicaragua.

Serikali ya Nigaragua imesema shule 1,700 zimefungwa na watu 30,000 wamehamishwa kutoka maeneo yote ya pwani yaliyo kwenye hatari ya kupata madhara kutokana na kimbunga hicho.

The post Kimbunga Eta chaipiga pwani ya Nicaragua appeared first on Bongo5.com.