Makamu wa Rais mteule wa Marekani, Kamala Harris aliposti kipande cha video katika ‘Insta story’ akionesha kufurahishwa na matokeo ya uchaguzi, kwenye hiyo video ameonekana akimpigia simu Joe Biden ambaye ameshinda kiti cha urais na kumwambia kuwa wamefanikiwa.

Kamala Harris ametengeneza historia katika taifa hilo lenye nguvu kubwa za kiuchumi duniani kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa RaisMarekani, mwanamke wa kwanza mwenye asili nyeusi na wa kwanza South Asian kukalia kiti hicho.

”Tumefanikiwa Joe,” Kauli ya Makamu Rais Kamala Harris akionekana kuwa mwenye furaha huku akiongea na simu akimwambia Rais mteule Joe Biden kuwa wameweza kufanya kile walichokusudia na wamefanikiwa katika hilo.

Joe Biden na Kamala wanaingia madarakani huku wakikutana na changamoto ya kwenda kufanya pale White House hasa kukabiliana na Janga la Virusi vya Corona ambalo limeua idadi kubwa ya Wamarekani, uchumi wa taifa hilo na matatizo ya BlackLivesMatter,

https://bit.ly/3pbnJOm

The post Kauli ya kwanza ya Makamu Rais Marekani Kamala baada kusikia ameshinda appeared first on Bongo5.com.