Baba mzazi wa mchezaji bora duniani, Lionel Messi ambaye pia ni wakala wake amekana taarifa zinazo sambaa kwamba mshambuliaji huyo ana mipango ya kujiunga na Paris Saint-Germain kutoka Barcelona msimu ujao na kuziita za uongo.

ONLITE - Messi n'ira pas au PSG !

Mchezaji huyo wa Argentina amekuwa akizungumzwa mno tangu alipotangaza binafsi anahitaji kuondoka Camp Nou mwezi Agosti.

Licha ya Messi na klabu yake kukaa mezani na kupata suluhu ya mgogoro wao lakini mambo yanaonekana hayajakaa sawa.

Kocha wa Manchester City ambaye pia amewahi kumfundisha Leo akiwa Barca, Pep Guardiola amehusishwa kuelekea PSG hivyo wawili hao kuwa katika klabu moja msimu ujao kwa mujibu wa ESPN.

Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti, mawasiliano tayari yameshafanyika baina ya Mabingwa hao wa Ufaransa na baba mzazi wa Messi ambaye ndiyo wakala wake ili kufanikisha usajili huo mwezi Januari.

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

The post Je Messi kutua PSG ?, baba mzazi afunguka appeared first on Bongo5.com.