Mapema siku ya Ijumaa Rais Trump alizungumzia uchaguzi wa Marekani na kutoa msururu wa madai hadhaa ya udanganyifu kuhusu zoezi hilo bila kutoa ushaidi.

 

Tumetathmini baadhi ya madai hayo.

Section divider

Trump: “Nimekuwa nikizungumzia upigaji kura kwa njia ya posta kwa muda mrefuUmeharibu vibaya mfumo wetuNi mfumo wa kifisadi na unafanya watu kuwa wafisadi.”

Bwana Trump ameweka zaidi ya ujumbe 70 kwenye Twitter akitilia shaka upigaji kura kwa njia ya posta, akiashiria kura “zimeibwa” tangu uchaguzi wa mwezi Aprili.

Lakini hakuna ushahidi wa kubainisha mfumo huo unaendekeza ufisadi.

Udanganyifu katika uchaguzi ni nadra sana nchini Marekani – kiwango cha udanganyifu ni chini ya asilimia 0.0009%, kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na mwaka 2017 na Kituo cha Haki cha Brennan Center. Hakuna ushahidi unaoashiria kumekuwa na udanganyifu katika uchaguzi huu wa sasa.

Rais mwenyewe ashawahi kupiga kura kwa nji aya posta. Alikuwa akiishi nje ya Jimbo la Florida alipojisajili kama mpiga kura wakati huo na kuomba apige kura kwa njiaya posta.

Mpango huo unajulikana kama kura ya utoro, ambao Bw. Trump aliunga mkono kwasabau aliamini ni salama.

Lakini ametofautiana na mfumo huo wa upigaji kura hasa pale majimbo yalipoamua kuwatumia watu makaratasi ya kupiga kura moja kwa moja

Majimbo ya Oregon na Utah yamekuwa yakitumia mfumo huo wa upigaji kura bila matatizo yoyote katika chaguzi zilizopita.

Section divider

Trump: “Walituma mamilioni ya makaratasi ya kupiga kura bila kuchukua hatua ya kuthibitisha uhalali wake.”

Wapiga kura waliosajiliwa katika majimbo tisa (pamoja na Washington DC) walitumiwa moja kwa moja makaratasi ya kupiga kura bila ya wao kuomba kutumiwa makaratasi hayo. Majimbo matano kati ya hayo yalikuwa yameweka hatua ya kukabiliana msambao wa virusi vya corona

Lakini majimbo manane kati ya hayo tisa – Colorado, Hawaii, Oregon, Utah, Washington, California, New Jersey, na Vermont – kwa sasa hayajapinga mfumo huo.

Usalama wa mifumo yote ya upigaji kura kupitia posta imeimarishwa – kama vile mamlaka kuhakikisha kura inaambatana na anwani ya sanduku la posta la mpiga kura alitesajiliwa pamoja na saini ya uthibitisho kwenye bahasha.

Upigaji kura kwanjia ya posta sio jambo geni- mfumo huo umetumika katika chaguzi nyingi.

Section divider

Trump: “Inashangaza jinsi kura zilizopigwa kupiti aposta ni za upande mmoja pekee.”

Rais Trump mara kwa mara amekosoa mpango wa kupanua mfumo wa upigaji kura kwa njia ya posta, akisema – bila ushahidi – unachangia “udanganyifu wa hali ya juu.”

ALitoa wito kwa wapiga kura wa Republican kujitokeza kwa wingi katika vituo vy a kupigia kura siku y auchaguzi, badala ya kutumia mfumo wa upigaji kura kwa njia y aposta.

Kuna ushahidi waliitikia wito wake kutokana na hali inayoshuhudiwa katika shughuli ya kuhesabu kura- Democratic wamefaidika pakubwa kutokana na kura zilizopigwa kwa nji aya posta huku Warepublican wakipiga kura zao ziku y auchaguzi.

SHughuli ya kuhesabu kura haijakamilika lakini katika Jimbo la Pennsylvania, inakadiriwa zaidi ya kura milioni 2.5 zilipigwa kwa njia ya posta, wafuasi wa Democratic walijitokeza mara tatu zaidi ya Republican kupiga kura

Section divider

Trump: “Katika Jimbo la Georgia, bomba la maji lilipasuka mbali na mahali kura zinahesabiwa lakini shughuli ya kuhesabu kura ikasitishwa kwa saa nne.”

Huo si ukweli.

Bomba la maji lilipasuka katika shamba lililoko karibu na chumba ambako kura zilikuwa zinajumuishiwa.

Hii hapa taarifa iliyotolewa na maafisa wa jimbo hilo press release.

Section divider

Trump: “Sasa yamesalia majimbo machahe ambayo hayajatangaza matokeo ya uchaguzi wa uraisMifumo ya uchaguzi ya majimbo hayo inaendeshwa na Democrats.”

Huo si ukweli “kimsingi”.

Katika Jimbo la Georgia, ambako matokeo hayajatangazwa, gavana na wabunge wa mabunge yote mawili ni wa Republican.

Waziri wa mambo nje wa Jimbo hilo, ambaye anasimamia masuala ya uchaguzi ni Brad Raffensperger ambaye ni mwanachama wa Republican.

Huu hapa ujumbe wake wa Twitter wa mwaka 2018 unaomuonesha Donald Trump akimuidhinisha.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Mfano mwingine ni kwamba, Nevada ina waziri wa mambo ya nje ambaye pia ni msimamizi wa maswala ya uchaguzi kutoka chama Republican

Section divider

Trump: “Hawangeruhusu waangalizi wanaoruhusiwa kisheria”

Rais Trump anazungumzia waangalizi wa uchaguzi. Hawa ni watu waliopo ndani ya vituo vya kuhesabu kura kwa lengo la kuhakikisha uwazi unazingatiwa.

Watu hao wanaruhusiwa katika majimbo mengi, lakini wanastahili kusajiliwa kabla ya siku ya uchaguzi, mara nyingi wanamwakilisha mgombea au chama, japo hali nitofauti katika baadhi ya majimbo.

Trump anahoji madai kwamba waangalizi wa Republican wamezuiliwa kufanya shughuli zao katika majimbo yanayosimamiwa na viongozi wa Democratic katika miji kama vile Philadelphia na Detroit.

Lakini waangalizi wa uchaguzi waliruhusiwa kushuhudia kura zinavyohesabiwa katika miji yote miwili.

Idadi wa waangalizi wa uchaguzi wanaoruhusiwa katika kituo cha kuhesabu kura inategemea ukubwa wa kituo hicho. Udhibiti huo huwekwa kabla ya uchaguzi.

Katika baadhi ya maeneo idadi ya waangalizi inadhibitiwa, kama sehemu ya hatua ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona. Pia idadi ya waangalizi imedhibitiwa kuzuia vitisho.

Katika mji wa Detroit, zaidi ya waangalizi 130 wanaowakilisha Democrat na Republican waliruhusiwa katika vituo vya kuhesabu na kujumuisha kura.

Karani wa mji huo Janice Winfrey amesema hana habari kuwa waangalizi wa Republican wanatolewa.

Katibu wa mji huo Janice Winfrey amesema hana habari kuwa waangalizi wa Republican wanatolewa.

Kitika Jimbo la Philadelphia, kuna video ambayo imekuwa ikisambazwa mitandaoni ikimuonesha mwangalizi aliyeidhinishwa akitolewa katika kituo cha kupiga kura, lakini kama ilivyoripotiwa, hatua hiyo ilitokana na mkanganyiko kidogo na baadaye aliruhusiwa kuingia.

Katika Jimbo la Philadelphia, kuna video ambayo imekuwa ikisambazwa mitandaoni ikimuonesha mwangalizi aliyeidhinishwa akitolewa katika kituo cha kupiga kura, lakini kama ilivyoripotiwa, hii ilikuwa kutokana na mkanganyiko wa masharti baadaye aliruhusiwa kuingia.

Waziri wa mambo ya nje wa Pennsylvania Kathy Boockvar amesema: “Kila mgombea na kila chama cha kisiasa kinaruhusiwa kuwa na mwakilishi katika kituo cha kura ili kushuhudia mchakato wa uchaguzi.Baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na Philly yanaonesha mubashara mtandaoni shughuli ya kuhesabu kura, kwa hivyo watu wanafuatili amchakato huu bisha shaka.”

The post Hotuba ya Trump ya dakika 17 akituhumu zoezi la upigaji kura yachunguzwa appeared first on Bongo5.com.