MwanaHipHop Roma Mkatoliki ameeleza kuwa anapata hofu sana kwa watoto wanaozaliwa na kulelewa kwa sasa kwa sababu kesho yao ya mahusiano itakuwa na changamoto kubwa kutokana na mapenzi ya siku hizi yamekuwa rahisi.

 

Akifunguka hilo kupitia post yake aliyoweka kwenye mtandao wa Instagram na Twitter Roma Mkatoliki ameandika kuwa 


"Napata hofu sana na watoto wetu tunaowazaa na tunaowalea kwa sasa, kesho yao ya mahusiano itakuwa na changamoto kubwa sana, mahusiano au mapenzi yamekuwa rahisi siku hizi, yaani hakuna kutongozana mnajikuta tu mmeshaanza mahusiano" ameandika Roma Mkatoliki 


"Unakuta kwenye party ya mwamba kuna pisi 8 na zote zinajijua zina-date na huyo mwamba halafu fresh tu daah, hivi ni pisi zipo cheap au wanaume tumekuwa cheap" ameongeza