Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kulitengeneza baraza lake la Mawaziri ambalo litahudumu kwa awamu ya pili ndani ya uongozi wake ambapo anamaliza awamu hii ya pili.

Mbali na yeye kuchaguliwa na wananchi kuhudumu katika nafasi yake ya Urais kwa awamu ya tano kwa ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 80 na anayemfuatia akiwa na aslimia 13 tu, alimpitisha Mama Samia Suluhu Hassan kuwa makamu wake wa Rias kwa awamu ya pili huku Kassim Majaliwa akiteuliwa kushika nafasi yake akiwa Waziri Mkuu ambapo siku ya jana ndio alipendekezwa na Rais Magufuli huku wabunge wote kwa asilimia 100 wakimpitisha kuendelea kulitumikia taifa la Tanzania.

Mbali na hao Rais Magufuli alimteua Prof. Adelardus Lubango Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baada ya hapo siku ya leo amewateua Mawaziri wawili ambao ni Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lakini pia amemteua Dkt. Philip Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, teuzi zote hizo zitanza leo Novemba 13, 2020.

Ukiachana na hao Mawaziri tayari Bungeni Spika wa Bunge na Naibu wake wanajulikana baada ya kuchaguliwa na Wabunge wote ambao ni Job Ndugai akiendelea katika nafasi yake kama Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano huku Dkt. Tulia Ackson akiendelea na nafasi yake pia ya Unaibu Spika akishika nafasi yake ile ile.

The post Hawa ndio viongozi ambao tayari Rais Magufuli ameshawateua kushika nyadhifa mbalimbali appeared first on Bongo5.com.