Mwanamuziki maarufu nchini Tanzania Diamond Platnumz hatimaye amekutana na watoto wake kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2018.

Aliyekuwa mke wake Zari aliwasili Tanzania Alhamisi usiku pamoja na watoto wao Tiffah na Nillan.

Picha za Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinamuonesha Diamond Platnumz akiwalaki watoto wake wawili.

Baada ya watoto hao kupokelewa, mmoja aliulizwa na wanahabari "umemletea nini baba na bibi yako?" na kujibu ‘’Pizza’’.