Rais John Magufuli ameapishwa leo Alhamisi Novemba 5, 2020 kuendelea na wadhifa huo kwa mhula wa pili.

Ameapishwa katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma katika tukio lililoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Baada ya kula kiapo na kusaini hati ya utii alikabidhiwa katiba na mkuki na ngao.

Mbali na Rais Magufuli, makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan naye alikula kiapo.