Gwiji wa zamani wa mpira wa miguu Duniani, Diego Maradona amefanyiwa upasuaji mzuri wa ubongo hapo jana na hali yake kwasasa inaendelea vizuri.
Nyota wa zamani wa Argentina, Diego Maradona .
Maradona mwenye umri wa miaka 60, alilazwa kliniki ya Ipensa huko La Plata, Argentina Jumatatu akiugua upungufu wa damu na maji mwilini.
Baadaye nyota huyo alihamishiwa kwenye Kliniki ya Olivos huko Buenos Aries ili kufanyiwa upasuaji kwenye hematoma ambapo kulikuwa na mkusanyiko wa damu kati ya utando na ubongo wake.
“Niliweza kufanya upasuaji kwa mafanikio na Diego alivumilia upasuaji vizuri sana,” alisema Leopoldo Luque, daktari binafsi wa Diego Maradona.
“Hatua ya sasa ni uchunguzi na itategemea jinsi hali itakavyokuwa ingawa sio ngumu sana, lakini bado ni kutwafanyika upasuaji mwingine wa ubongo.”
Maradona, ambaye alishinda Kombe la Dunia na Argentina mnamo 1986, anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora na wakubwa wa wakati wote.
Kocha huyo wa Gimnasia Esgrima, kwa kara ya mwisho alionekana hadharani katika siku yake ya kuzaliwa siku ya Ijumaa iliyopita kabla ya mechi ya ligi ya timu yake dhidi ya Patronato.
The post Diego Maradona afanyiwa upasuaji wa Ubongo, mashabiki walala nje ya hospitali (+Video) appeared first on Bongo5.com.