David Beckham anataka mchezaji wa zamani wa Real Madrid Sergio Ramos kuichezea Inter Miami wakati kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 itakapokamilika msimu ujao.. (AS)
Kiungo mshambuliaji wa Manchester City na England Phil Foden , 20 anatarajiwa kupatiwa mkataba mpya ambao utaongeza mara tatu mshahara anaopata kwa sasa.(Star on Sunday)
West Ham United inatarajiwa kuwasilisha ombi la £30m kumnunua mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele iwapo klabu hiyo ya ligue 1 itaamua kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Sun on Sunday)
Meneja mkuu wa klabu ya Lyon Vincent Ponsot amefichua kwamba Arsenal ni miongoni mwa klabu tatu mbazo zilikuwa zinamnyatia kiungo wa kati wa Ufaransa Houssem Aouar katika dirisha la uhamisho lililopita lakini ilitoa dau la chini ya thani ya mchezaji huyo mwenye umri wa kiaka 22.. (Sport Witness)
Bayer Leverkusen ilikataa kuanzisha mazungumzo na Man United kuhusu uwezekano wa kumuuza winga wa Ufaransa Moussa Diaby katika dirisha la uhamisho. (Bild, via Inside Futbol)
Aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal Lucas Podolski ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Uturuki ya Antalyaspor amekosoa Arsenal na mkufunzi wake Mikel Arteta kwa jinsi wanavyomfanyia Mesut Ozil, mchezaji mwenza wa Ujerumani.. (Bild, via Goal)
Kipa wa Argentina Sergio Romero, 33, anafanya mazoezi akiwa pekee katika klabu ya Man United akitumai kuwachiliwa kuondoka katika klabu hiyo kwa uhamisho wa bila malipo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Sun on Sunday)
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur na England Harry Kane, 27, anaamini Spurs ina fursa nzuri ya kushinda Premier League msimu huu.. (Sunday Mirror)
Mkufunzi wa klabu ya Rangers Steven Gerrard anasisitiza kuwa sasa sio wakati wa kuzungumzia mkataba mpya wa kiungo Steven Davis , mwenye umri wa miaka 35 anayechezea Ireland. (Scottish Herald)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta hajutii kumuuza kipa wa Argentina Emiliano Martinez, 28, katika klabu ya Aston Villa. (Sunday Mirror)
Marseille wamejiondoa katika ushindani wa kumsajili mchezaji wa Strasbourg mwenye thamani ya £20m Mohamed Simakan. (Birmingham Mail)
Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy alichunguza sana thamani ya beki wa kulia wa England kyle Walker ya £15m lakini akamruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anayeimarika katika klabu ya Southampton kuondoka kwa £12m mwezi August.
The post David Beckham amtaka Sergio Ramos, Inter Miami appeared first on Bongo5.com.