Taarifa kutoka nchini Kenya zinasema, Mtanzania aliyehukumiwa kwa kuhusika katika shambulio la kigaidi lililotokea mwaka 2015 katika chuo kikuu kimoja nchini humo na kusababisha watu 148 kufariki, amejiua mwenyewe akiwa gerezani.

Washambuliaji wanne waliuawa kwa kupigwa risasi na Wanajeshi wa Kenya katika chuo Kikuu cha Garissa, lakini Mtanzania huyo, Rashid Charles Mberesero na wenzake wawili walikamatwa na mwaka jana na kuhukumiwa kwa kuhusika katika ugaidi.

Hukumu hiyo ilimpa, Mberesero kifungo cha maisha gerezani.

Taarifa zinasema alikuwa na matatizo ya akili wakati akiwa gerezani na alikuwa anamuona mtaalamu wa afya akiwa gerezani.

Gazeti la Daily Nation linasema Mberesero alijinyonga mwenyewe akiwa gerezani kwa kutumia blanketi lake.