Mahakama ya Wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma imemhukunu kwenda jela miaka miwili pamoja na faini ya Milioni 5, Agnes Damian(40) mkazi wa Mji Mwema Manispaa ya Kigoma Ujiji baada ya kupatikana na hatia ya kumchanachana na wembe sehemu mbalimbali za mwili Binti wa miaka 15 ambaye ni mtoto wa mume wake.


Hukumu hiyo imetolewa leo Novemba 30 na Hakimu, Eva Mushi ambaye amesema l adhabu hiyo inapaswa kuwa fundisho na onyo kwa wanaotenda matukio ya kikatili hasa kwa watoto.


Agnes anadaiwa kutenda tukio hilo Juni 18, ambapo aliingia chumbani nakufanya ukatili huo akimtuhumu kuwa Binti huyo alimpiga mwanae hivyo lazima ampe onyo.


Kabla ya adhabu hiyo, Agnes aliomba kupunguziwa adhabu kwakuwa anatunza watoto wawili, ni yatima na hivi karibu amepona ugonjwa wa kupoza japo hajawa timamu asilimia mia moja.